banner

Monday, May 5, 2014

Mganga wa Diamond atoboa siri nzito juu ya tuzo 7 za Kili Music Awards 2014 alizopewa msanii huyo




Yule mganga maarufu wa mastaa nchini ambaye aliwahi kutangaza kuwa amekuwa na ukaribu na mwanamuziki Diamond ameibuka na kusema kuwa tuzo hizo saba alizozipata zinamaana kubwa sana kwenye kazi zake anazozifanya.
 

Akiongea na gazeti  la Makani Bongo kwa njia ya simu( 0788844490) toka Mwanza alikoalikwa na wananchi wa huko kwa ajili ya kutoa huduma, mganga huyo alisema:

 
"Niliongea na Diamond wiki moja kabla ya shoo nikamueleza kuwa atapokea tuzo nyingi sana mwaka huu na hizo tuzo ni ishara tosha ya kudumu kwenye game kwa miaka kama hiyo ya tuzo zake kwa maana ya miaka saba mbele  nyota yake itaendelea kung'ara" Alisema Dokta Kamdege  na  kuongeza:
 
"Unajuwa haya mambo ya maagano yapo. Muziki na miti shamba vinaendana kwani kwenye dunia hii ya leo maadui ni wengi kuliko marafiki, hivyo ni vyema ukalijua mapema hilo na kujikinga kama ilivyo kwa Diamond."

Mganga huyo alitoa uwito kwa watanzania popote walipo kuendelea  kupata huduma zake kwani hii ni kama baraka kwa taifa la Tanzania.
 
Credit: Gazeti la Mskani Bongo

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment