Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wa majeshi yake.
Amri iliyotolewa na Rais kupitia kwa
televisheni, ilisema kuwa Generali James Hoth Mai ataondolewa katika
wadhifa wake mara moja.Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na vurugu tangu mwezi Disemba.
Wiki jana waasi waliuteka mji ulio na utajiri mkubwa wa mafuta Bentiu.
Mbali na hayo, umoja wa mataifa ulitoa ripoti iliyohusisha wapiganaji waasi na mauaji ya kikabila.
Na pia imekosoa serikali kwa kutoa taarifa za kupotosha kuhusu mauaji ya halaiki yaliyofanyika mjini Bentiu punde waasi walipouteka mji huo. Mamia wanaaminika kuuawa.
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini,Michael Lueth, hakuwa mkweli alipowaambia wandishi wa habari kuwa wakazi waliokuwa wanatafuta hifadhi katika makao ya Umoja wa Mataifa walizuiwa kuingia katika hifadhi hiyo.
Baada ya waasi kuuteka mji wa Bentiu waliwalenga mamia ya raia wasio na hatia na ambao walikuwa wametafuta hifadhi ndani ya msikiti, kanisa na hospitali na kuwaua kwa misingi ya ukabila
Hata hivyo waasi wanaomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais Riek Machar wamekanusha madai ya UN kuwa walihusika na mauaji ya mamia ya raia wasio na hatia huku vituo vya redio katika mji huo vikitumiwa kueneza chuki.
0 comments:
Post a Comment