banner

Saturday, May 3, 2014

Ripoti ya polisi wa Kenya kuhusu gari la Freeman Mbowe kukamatwa nchini humo likihusishwa na ugaidi



Kwenye magazeti ya April 30 2014 Tanzania miongoni mwa stori kubwa ilikua ni hii ya kukamatwa kwa gari la kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni ambae pia ni mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe ambapo baadhi ya vichwa vya habari vilisema ni kutokana na kuhisiwa kutumika kwa ugaidi.

Mtangazaji  Millard Ayo  amepata  nafasi ya kuzungumza na msemaji wa Polisi nchini Kenya Gatiri Mboroki anaethibitisha kwamba ni kweli gari la Mbowe lilikamatwa tarehe 25 April 2014 ambapo gari hilo baada ya kuvuka mpaka kuingia Kenya likitokea Tanzania lilibadilishwa namba.

Anasema kutokana na visa vya ugaidi nchini Kenya baada ya Wananchi kuona gari imebadilishwa namba na kupaki kwenye hoteli wakaripoti Polisi, Polisi walikwenda na kumkuta dereva peke yake aliewaambia kwamba kiongozi wa chama ambae ni Freeman mwenye gari amekwenda Nairobi kwa ndege, hiyo ilileta utata kidogo kwa kujiuliza amekwenda Nairobi kwa ndege iweje aache gari?’

Baada ya hapo gari lilipelekwa kwenye kituo cha polisi na Mh. Mbowe akaambiwa aende kujitambulisha ambapo kweli alifika kituoni na kujitambulisha akiwa na Mh. Wenje na baada ya hapo waliruhusiwa na kupewa gari wakaondoka muda mfupi baadae
 
 
Kwa kumalizia Gatiri Mboroki amesema hakuna aliefungwa wala gari hilo halijawahi kutumika kwenye visa vya ugaidi nchini Kenya na wala halikuzuiliwa isipokua sababu pekee ya gari hilo kupelekwa Polisi ni baada ya kuonekana likibadilishwa namba.

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment