Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe amewatoa
wabunge wote wa upinzani Bungeni ikiwa ni shinikizo la kuipinga Bajeti
ya Wizara ya Nishati na Madini kama ilivyokuwa imewasilishwa na Waziri
wa Wizara hiyo Professa Sospeter Muhongo.
“Hatuwezi kuendelea kuzungumzia bajeti ya Serikali
isiyokuwa na sera,mimi kama Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni
siwezi kuendelea kuiongoza kambi inayoburuzwa,”
amesema Mbowe na kuongeza:
“Tunawaachia bungeni lenu mpitishe bajeti yenu ili siku zijazo mkutane na hasira za wananchi,kwakuwa haya mlishayapanga”.
0 comments:
Post a Comment