banner

Saturday, May 24, 2014

JB na Steve Nyerere wazinguana msibani kisa pesa.....Wakiwa katika mabishano makali, JB atandikwa ngumi tisa na kudondoka chini



Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua wasanii Jakob Steven Jb na Steve Magele Nyerere wamepigana  ngumi kavukavu karibu na eneo la msiba wa marehemu Adam Kuambiana huko Bunju huku kisa kikiwa kugeukana kwenye dili la matangazo.

Kwa mujibu wa tovuti ya maskanibongotz, msanii steve nyerere ndiye aliyeanza kumchokoza msanii Jb kwa kumchana baada ya kumgeuka kwenye mchongo wa matangazo ya kampuni moja ya simu iliyopo maeneo ya Moroco Jijini Dar.

Habari zaidi zilisema wakati wasanii hao wakiwa baa wanakula kilaji siku moja kabla ya mazishi ya msanii mwenzao, Steve alimvamia Jb na kuanza kumchana na kumueleza jinsi alivyokuwa na roho mbaya kwa kumgeuka kwenye mchongo wa mtangazo ya simu pale Moroco ..

Majibizano hayo yalidumu kwa muda mrefu  huku Jb akiwa kimya kwani stevu alionekana kuumizwa na jambo hilo kwani inadaiwa zile picha za Jb kwenye mabango ya mtandao huo wa simu mchongo alipewa  steve lakini baadae Jb alimgeuka na kwenda kupiga mchongo kimaya kimya na kumuacha Steve akishangaa.

Steve aliendelea kumsasambua Jb mbele ya watu, hali  iliyomfanya Jb kunyanyuka na kuanza kumfokea huku akimtishia kumfinyangafinya na ufupi wake ndipo steve nyerere aliyekuwa ameshika chupa ya kilaji aliruka kichwa kimoja kilichompiga Jb kifuani na kupepesuka.

Wakati watu akijianda kwenda kuamulia basi Steve ambae aliwahi kucheza ngumi miaka ya nyuma alimshindilia Jb ngumi kama tisa za harakaharaka sehemu ya tumbo, hali iliyomfanya Jb kudondoka chini na kushindwa kupumua kwa dakika tano kisha alinyanyuka na kukalia kiti.

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment