Badhi ya wajumbe wa Bunge maalum la Katiba walio katika Umoja wa UKAWA jioni ya leo wameamua kutoka nje wakati wajumbe wakiendelea na majadiliano ya taarifa za kamati ya bunge hilo kuhusu sura ya kwanza na ya sita.
Hatua hiyo imefikiwa na wajumbe hao baada ya kuunga mkono mchango wa Profesa Lipumba ambaye amesikitishwa na jinsi mjadala wa bunge hilo unavyogubikwa na ubaguzi.
Profesa Lipumba amesema wanahitaji katiba itakayo hakikisha kila mwananchi anapata haki yake bila kujali rangi jinsia na makabila msingi alioucha baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Aidha Profesa Lipumba alieza kuwa amesikitishwa na Kauli iliyotolewa na Waziri William Lukuvi wakati wa sherehe ya kumsimika mchungaji Joseph Bundala kuwa Askofu akimwakilisha Waziri Mkuu
Msikilize Hapa:
http://www.hulkshare.com/timesfmradio/lipumba-bunge-la-katiba
0 comments:
Post a Comment