VIJANA wawili waliokuwa katika pikipiki aina ya Boxer wamenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali eneo la Kijitonyama baada ya kumpora dada mmoja mkoba.
Vibaka hao walifanikiwa kumpora dada huyo aliyekuwa akitembea kwa miguu akitokea Benki ya Access katika maeneo ya showroom ya Akachube iliyopo Kijitonyama jijini Dar.
Wakati wa uporaji huo, alikuwepo msamaria mmoja aliyekuwa na gari aina ya Toyota Carina aliyefanikiwa kuwasukumia mtaroni na gari lake ambapo wananchi walianza kuwashushiwa kichapo cha kufa mtu.
Kipondo kiliendelea mpaka askari wa jeshi la polisi walipofika na kuwanusuru.
0 comments:
Post a Comment