banner

Friday, May 9, 2014

Picha kutoka Bungeni mjini Dodoma leo...


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu maswali ya wabunge wakati alipohitimisha hoja ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, bungeni mjini Dodoma Mei 9, 2014.

Spika wa Bunge Mhe.Anna Makinda akiwa anaendesha kikao cha Bunge leo wakati wa majadiliano ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na TAMISEMI.

 
Wabunge wakifuatilia mjadala ndani ya Bunge.

 
Spika wa zamani ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Africa Mashariki Mhe.Samweli Sitta kushoto akijadiliana jambo na Spika wa Bunge Mhe.Anna Makinda Mara baada ya Bunge kuahirishwa hadi jioni leo. 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipongezwa na Mkewe Tunu baada ya Bunge kupitisha bajeti ya Ofisi yake mjini Dodoma Mei 9, 2014. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Pudenciana Kikwembe na watatu kushoto ni mbunge wa Temeke, Abas Mtemvu.

 
 Waziri Mkluu, Mizengo Pinda akipongezwa na katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Florens Turuka baada ya bunge kupitisha bajeti ya Ofisi yake mjini Dodoma Mei 9,2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment