Polisi akilinda sehemu ya shehena ya meno ya tembo iliyokamatwa Dar es Salaam hivi karibuni.
Meno ya tembo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya vielelezo mahakamani yalitoweka katika Kituo cha Polisi cha Kilwa mkoani Lindi. Tukio hilo limenukuliwa katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ikisema meno makubwa 108 ya tembo na kilo 20 za meno mengine ya tembo yaliyokuwa yamehifadhiwa kama kielelezo cha kesi za uhujumu uchumi, yamebainika kutoweka kinyemela.
Ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni juzi, imebainisha kuwa meno
mengine makubwa ya tembo yaliyokuwa na uzito wa kilo 498.3
yamebadilishwa kinyemela na meno madogo, hivyo kusababisha hasara ya
kilo 203.66 za meno ya tembo ambazo thamani yake haikufahamika.CAG
Ludovick Utouh katika ripoti hiyo ya mwaka ulioishia Juni 30, 2013,
amebainisha kuwa kumbukumbu katika Pori Tengefu la Miguruwe zilionyesha
kuwa katika kipindi cha kuanzia Juni 5 hadi Juni 8, 2012 meno makubwa
108 yalikuwa miongoni mwa vielelezo kituoni hapo.Kati
ya meno hayo 108 yaliyokamatwa katika matukio ya ujangili, 74
yalitoweka katika kituo cha polisi wakati 34 yalibadilishwa na meno
madogo, tofauti na yale yaliyokuwa yamekamatwa yakihusishwa na kesi ya
ujangili Na. 3/2009 na kesi nyingine ya uhujumu uchumi Na. 2/2010 ambazo
zilikuwa zikiendelea mahakamani mkoani Lindi.
Pia ilibainika kuwa kilo 20 za meno ya tembo ambayo yalikamatwa na
kuhifadhiwa kama kielelezo cha majalada KLM/IR/184/2009, KLM/IR/235/2009
na KLM/IR/567/2010 yalitoweka.
Gari la ujangili latowekaUkaguzi huo pia ulibaini kuwa gari
lililokamatwa likiwa kielelezo baada ya kukutwa na kilo 26 za meno ya
tembo yenye thamani ya Sh135 milioni liliondolewa kinyemela katika Kituo
cha Polisi Kilwa.CAG katika ukaguzi huo alibaini upungufu katika
usimamizi wa meno ya tembo na nyara nyingine za taifa katika chumba cha
meno hayo Dar es Salaam na vituo vya mikoani.CAG katika taarifa yake
hiyo amesema kutokana na kukosekana kwa kumbukumbu sahihi, meno ya tembo
yanaweza kuibwa au kupotea bila menejimenti kuwa na taarifa yoyote,
hivyo ameishauri Serikali kuhakikisha kunakuwa na udhibiti wa kutosha
katika usimamizi wa nyara za Serikali nchi nzima.
MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment