Tanzania kwa mara ya Kwanza imesema inayo uhakika kuwa waasi wa
M23 walioondolewa nchini Jamuhuri ya Kongo ni raia Rwanda. Waziri wa
Mambo ya Nje Benard Membe ameliambia Bunge la Tanzania kuwa anao uhakika
kuwa waasi wa M23 walitokea nchini Rwanda.
Hii ni Mara kwanza kwa Tanzania kukiri hadharani kuwa inao uhakika kuwa waasi hao ni raia wa Rwanda.
Matamshi hayo ya Waziri huyo aliyatoa wakati alipokuwa akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara yake ambapo pia alikiri kuwa bado uhusiano wa Tanzania na Rwanda sio mzuri.Hata hivyo upande wa Upinzani ulishambulia Waziri Membe ukidai kwamba Waziri huyo anachochea kuvurugika kwa uhusiano wa Watanzania na Rwanda kwa kuhisi kuwa M23 ni Wanyarwanda nahata kutaka achukuliwe adhabu kali.
Mbali na tuhuma hizo Waziri Membe alizidi kusisitiza kuwa waasi wa M23 ni raia wa Rwanda akisema hiyo ni ripoti ya Umoja wa Mataifa.
Mbali na waziri, baadhi ya wabunge walimuunga mkono waziri Membe kuwa waasi wa M23 ni raia wa Rwanda.
0 comments:
Post a Comment