banner

Wednesday, May 28, 2014

Wizara ya Ardhi, nyumba na mkazi Yazua Gumzo Bungeni

 
 
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeitaka serikali kusitisha zoezi la ugawaji wa ardhi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi mpaka pale itakapobainika ni kiasi gani cha ardhi kilichopo kwa wawekezaji,ili kuepusha migogoro ya ardhi nchini ambayo inaendelea kusababisha vifo vya watanzania wasio na hatia
 
Hatua hii inakuja huku waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka akikanusha vikalia uwepo wa migogoro ya ardhi kwa kile anachokiita ukosefu wa tekinolojia. 
 
Ni katika Mkutano wa kumi na tano kikao cha ishirini Halima Mdee Msemaji kutoka Kambi Rasimi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni waziri kivuli wa Wizara ya Ardh Nyumba na Maendeleo ya makazi anasimama na kusema tathmiini hiyo ikifanyika kwa kiasi kikubwa itapunguza migogoro miongoni mwa wananchi na wawakezaji hasa wa kigeni
 
Esther Bulaya ni Mjumbe kutoka kamati yaBunge Maliasili na mazingira kwa niaba ya kamati hiyo anasistiza kufuata kwa sheria katika kutoa vibali vya ujenzi wa magorofa nchini.

Tarehe 27 mwezi huu waziri mwenye Dhamana ya  wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Prof Anna Kajumulo Tibaijuka aliwasilisha makadirio ya Mapato na matumizi kwa wizara yake na akaomba shilingi bilioni 11.5 kwa ajili ya mishahara, matumizi mengineyo  bilioni 42.

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment