Mamia ya wapenzi na washabiki wa klabu kongwe ya mpira wa miguu
hapa nchini Simba leo mchana wamejikusanya kwa wingi katika makao makuu
ya klabu yao hiyo,kupinga Michael Wambura kuondolewa kwenye orodha ya
wagombea kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Wanachama
hao ambao walizunguka jengo hilo na kutaka wapewe sababu za msingi
kwanini Wambura ameondolewa huku wakitaka kufanya vurugu lakini vyombo
vya usalama waliwahi kufika eneo la tukio na kuweza kuwatuliza wanachama
Hao.
Polisi wakiwa wamefika eneo la klabu ya simba ili kuimarisha
ulinzi na kuwataka wanachama wa simba kutulia ili wapate majibu kwa
kamati ya uchaguzi.
Wanachama wa simba wakiwa wamelizunguka Jengo la klabu yao mchana
huu kupinga kuondolewa kwa wambura kwenye uchaguzi wa klabu hiyo
0 comments:
Post a Comment