banner

Tuesday, May 6, 2014

Taarifa ya jeshi la polisi mkoani Mwanza kuhusiana na Bomu lililolipuka ndani ya kanisa la KKT Makongoro na kujeruhi mtu mmoja


Mmoja wa majeruhi wa  bomu la kutengenezwa ‘kienyeji’ ambao ulilipuka katika vyumba vya Hosteli za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T), mtaa wa Gana jana  saa mbili  usiku.
*************
Mtu mmoja amenusurika kufa baada ya kulipukiwa na bomu lili lotengenezwa kienyeji kisha kuhifadhiwa katika mfumo wa zawadi na kutegwa katika nyumba ya kupumzikia wageni iliyopo kanisani la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo.

Majeruhi huyo ambaye ni mhudumu wa nyumba hiyo Benadeta Alfred amelazwa katika hospitali ya Rufaa Bugando ambapo anapatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya sehemu kubwa ya mwili wake

Kutokea kwa mlipuko huu wa  bomu katika eneo hili la kanisa kunaacha maswali mengi kwa wakazi wa jiji la Mwanza na waumini wa kanisa hili
 


 
Bomu hili lilowekwa kwa mfumo wa zawadi ndani ya nyumba ya kupumzikia linadaiwa kuwa hapa kwa mda wa siku tatu bila kufahamu mwenye mzigo huu na kilichomo ndani yake

Licha ya uimara wa fensi na ulinzi uliopo katika eneo hili la kanisa maswali mengi yanaibuka juu ya mhusika aliyeingiza bomu hilo na kwa njia gani.

Kikosi maalum cha uchunguzi wa milipuko kimewasili kutoka jijini Dar es salaam kufanya uchunguzi katika eneo hili la mlipuko.

Aidha wito umetolewa kw awananchi wote kuwa makini na vitu wasivyovijua ili kujiepusha na madhara kama haya.

Juhudi za kunusuru maisha ya Benardeta zinaendelea hapa katika hosptali ya rufaa ya Bugando katika chumba cha ungalizi maalumu.

Matukio ya milipuko inayosadikiwa kuwa mabomu imeendelea kurindima nchini hasa katika mikoa ya Arusha, visiwani Zanzibar na sasa jijini Mwanza, hali ambayo inaacha swali kwa jeshi la polisi juu ya usalama wa raia katika maeneo yasio rasmi na ya umma.

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment