banner

Tuesday, May 6, 2014

Taarifa mpya kuhusu Mabasi yaendayo kasi Dar es salaam….

gar

Unaambiwa Zaidi ya daladala 1,800 hazitoruhusiswa kufanya safari zake maeneo ya katikati ya jiji la Dar baada ya miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka kukamilika na ujenzi huo wa miundombinu hiyo inatarajiwa kukamilika mwisho wa mwaka huu ambapo mabasi 10 madogo na makubwa 20 yatatoa huduma za awali kama majaribio.

Meneja wa uendashaji wa Dart Peter Mnuo amesema Huduma hii ya majaribio inategemewa kutolewa December mwaka huu na huduma kamili itaanza kutolewa kuanzia July 2015,wakala wa mabasi hayo yaendayo haraka umekwishaanza maandalizi ya kutoa huduma ya awali ya mabasi makubwa kuanzia Kimara Mwisho hadi Kivukoni ikiwa kama sehemu ya mfumo wa kuanza kutoa huduma.

gar1

Mabasi hayo ya majaribio yanaweza kubeba jumla ya abiria 140 hadi 160 mpaka hapo itakapoanza kutoka huduma kamili July 2015,mradi huu umepangwa kutekelezwa kwa awamu 6 ambapo kwa awamu ya kwanza unahudumiwa na fedha kutoka Bank ya dunia.

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment