MAMIA ya wananchi wa shehia za Wawi, Wara na wapita njia wengine, jana wameshuhudia mwili wa marehemu
MOHAMMED
Soud Makame (17), ambae ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika skuli ya
sekondari Vikunguni, amekutwa amekufa
ndani ya nyumba iliyokuwa haijahamiwa katika mtaa wa Wawi wilaya ya Chake Chake Pemba.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, taatifa za tukio hilo zilitolewa na mtoto
mmoja ambae aliukuta mwili huo ndani ya nyumba hiyo, wakati yeye alipokuwa
akifukuza kuku.
Walisema
baada ya kuuta mwili huo, waliamua kutoa taarifa kwa vyombo husika ikiwa ni
pamoja na polisi, hospitali, sheha wa shehia ya Wawi na baadhi yao
kupiga simu kwa waandishi wa habari juu tukio hilo.
Walisema
waalimkuta marehemu akiwa na kitambaa ambacho wakati wa uhai wake alikuwa
akikivaa kichwani, ingawa kwa jana walikikuta kikiwa shingoni mwake, mithili ya
mtu aliejitia kitanzi.
0 comments:
Post a Comment