banner

Wednesday, April 23, 2014

Koramu yatimia bungeni.....Mjadala wa katiba mpya waendelea... Wajumbe wengine wa kundi la 201 warejea bungeni


Wakati bunge Maalum la Katiba linaendelea na kikao leo, baadhi ya wajumbe waliokuwa wanasemekana kuwa ni wanachama wa umoja wa kinachoitwa katiba ya wananchi (UKAWA) wamejitokeza na baadhi yao kukanusha kuunga mkono umoja huo.


Mjumbe wa Bunge la Katiba, Mhe.  Ezekiel Oluoch akiingia jana kwenye  kikao cha Bunge Maalum la Katiba  mjini Dodoma. Mhe. Uluoch, ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa Chama cha Walimu (CWT), ni mmoja wa wachangia mada wakubwa aliyejipatia umaarufu mkubwa mjengoni.


Mwenyekiti  wa Bunge Maalum la KAtiba Mhe.Samwel sitta akiliambia Bunge jana kuwa pamoja na UKAWA kuondoka koramu ya wabunge walio ndani ya ukumbi imetimia kwa hiyo mchakato wa katiba mpya utaendelea kama kawaida.



Mwenyekiti wa Kamati namba tano ambaye anatoka chama cha wananchi CUF Mhe.Hamad Rashid akichangia mjadala jana na kuliaminisha bunge kuwa pamoja na wanaojiita wana ukawa kutaka mfumo wa serikali tatu yeye anaamini mfumo wa serikali mbili na kuwashangaa wenzake kwa kuwa vigeugeu na kwamba maridhiano yatapatikana ndani ya bunge na si nje ya bunge.

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment