WATU 13 aiwemo askari wa kikosi cha
usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la
kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha
Ikungi mkoani Singida usiku wa kuamkia leo.
Ajali hiyo ilitokea baada ya ajali
ya kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga mwendesha baiskeli
aliyepoteza maisha papo hapo na wakati wananchi wakiwa wamekusanyika
eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea kupima ajali hiyo, lilitokea
basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu hao pamoja na trafiki na
kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza maisha eneo hilo.
Basi hilo lililokuwa likitokea
Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama eneo hilo mpaka dereva wake
alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida.
Miili 14 ya waliopoteza maisha
katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida
pamoja na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo.
0 comments:
Post a Comment