Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amebaini kuwapo kwa wanafunzi wanaopatiwa mikopo katika vyuo vitano nchini licha ya kufeli au kuahirisha masomo yao.
Kwa mujibu wa taarifa ya CAG ya ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha 2012/13, mikopo ya kiasi cha Sh. milioni 201.5 ilitolewa kwa wanafunzi hao.
Taarifa hiyo imevitaja baadhi ya vyuo na kiasi cha fedha kila kimoja kwenye mabano kuwa ni Vyuo Vikuu katika nchi za Algeria, Cuba ( milioni 132), Urusi (milioni 9.6), Chuo Kikuu cha Dodoma (milioni 43.9) na Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM) (milioni 28.9).
Pia, imebaini wanafunzi kupewa mikopo bila kuzingatia matokeo ya mitihani yao kama ilivyoainishwa katika kanuni za fedha za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini ( (HESLB), hivyo kukosekana kwa fursa kwa wanafunzi waliostahili kupata mikopo.
Imeeleza kuwa hali hiyo imesababisha matumizi mabaya ya fedha kwenye vyuo na hasara kwa umma kutokana na Bodi kushindwa kukusanya fedha kutoka kwa walionufaika na mikopo hiyo.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment