Mkazi wa Kijiji cha Shilabela, mkoani Geita, ambaye amefahamika
kwa jina moja la Daud (35) amekufa kwa kujinyonga chooni kutokana na
ugomvi baina yake na mkewe…
Taarifa zilizopatikana zinadai Daud alikutwa amejinyonga chooni na kwamba, kabla ya kuchukua uamuzi huo alikwenda nyumbani kwa mama mkwe wake kupeleka matumizi kwa mkewe, Irene Jackson (18) ambaye anaishi kwao baada ya kutokea ugomvi wa kindoa.
“Alikuja jana (juzi) hapa akaniambia nina maongezi na wewe, nikamwambia anisubiri kwani muda ule nilikuwa naelekea sokoni kwa mama,” alisema Irene.
Irene alisema baada ya kutoka sokoni alimkuta mume wake akila chakula cha mchana na majirani na kwamba, alimweleza amepeleka matumizi ya mtoto na kumtaka wazungumze lakini mwanamke huyo alikuwa bado ana kazi.
“Nilikuwa na kazi zangu nikamwomba awe na subira, baadaye jioni niliporejea nikamkuta yupo akaniambia tuongee nikamwambia sasa hivi ni usiku arudi kesho tuongee,” alisema Jackson.
“Aliniomba kitenge changu, nikamwambia mwanangu mimi sina kitenge, akasema basi hata cha mke wangu, nikamwambia mke wako hana kitenge,” alisema Mama mkwe wa Daud.
Anasema baada ya kumweleza hivyo akaondoka na geti likafungwa saa 2:45 usiku na kwamba, alirejea tena saa 4:00 usiku na kuwagongea lakini hawakuamka.
“Baada ya muda mfupi kama nusu saa hivi, tukapewa taarifa kuwa mume wangu amejinyonga chooni,” alisema Irene.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alikiri kuwapo kwa tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi.
0 comments:
Post a Comment