Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) cha jijini
Mwanza, Helma Michael (22) ameuawa kwa kupigwa mawe na wanafunzi
wenzake, wakimhisi kuwa ni mwizi wa kompyuta ndogo za mkononi na deki
chuoni hapo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Valentino Mlowola, alisema juzi kuwa
mwanafunzi huyo aliuawa Mei 13 mwaka huu saa 4.00 usiku, katika eneo la
Nyamalango Malimbe, ambapo baada ya kubainika katika eneo hilo alianza
kupigwa kwa mawe, fimbo na mapanga hadi kusababisha kifo chake: “Huyu
ameuawa katika tuhuma ambazo mpaka sasa hazijathibitishwa,” alisema.
Kutokana na mauaji hayo, watu 17 wamekamatwa na Polisi imeanza
uchunguzi kuhusu tukio hilo huku Kamanda Mlowola akiwataka watu
kutojichukulia sheria mkononi kwa kuwaua watu ambao hawana hatia.
0 comments:
Post a Comment