banner

Sunday, May 25, 2014

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi akaidi Amri ya Rais Joyce kufuta matokeo ya uchaguzi….!

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi Justice Mbendera amekaidi Amri ya Rais Banda ya kufuta matokeo ya uchaguzi. Mbendera amewaagiza maofisa wa tume ya uchaguzi kuendelea na zoezi la kuhesabu kura na kuomba ushirikiano wao wa dhati katika kipindi hiki kigumu.
 
Amesema Rais hana mamlaka ya kuingilia tume ya uchaguzi ambayo inafanya kazi kikatiba na kisheria. Pia Rais Wa chama cha wanasheria wa Malawi (MLS) na Pia Mwanasheria Mkuu wa Zamani wa Malawi wameongea na Vyombo vya Habari Muda Mfupi uliopita na kusema ibara aliyoitaja Rais haimpi mamlaka ya kufuta uchaguzi..
  Wamesema kifungu cha 5 cha sheria ya uchaguzi wa Bunge na Rais kinaipa Mamlaka Jukumu lote tume ya uchaguzi kusimamia mchakato wa Uchaguzi. Pia kifungu cha 100 cha sheria hiyo kinatoa haki ya chama au mgombea kulalamika kwa tume kuhusu ukiukwaji wa Mwenendo wa Uchaguzi na kama ndani ya masaa 48 hali hiyo isiporekebishwa kwa kiwango cha kuridhishwa basi kifungu namba 113 cha sheria hiyo hiyo kitatumika kupeleka mashtaka Mahakama Kuu.
tume

Hata hivyo Mwanasheria mkuu akizungumzia Amri hiyo ya Rais leo hii amesema “Kuna Mtu anafanya uhaini hapa sasa” na kuendelea kudai kuwa Rais amefanya uhaini kwa kukiuka ibara ya 88 ya katiba ya nchi kutoa “Presidential Decree” bila sababu yoyote ya msingi inayozingatia katiba na mamlaka ya kisheria

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment