banner

Monday, May 26, 2014

Mkurugenzi wa zamani wa TANESCO afikishwa mahakamani kwa kosa la kuhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya milioni 884

 
                 Mhando (kushoto) na wenzake wakitoka mahakamani.

MKURUGENZI  wa zamani wa Shirika la Umeme nchini, (Tanesco) William Geofrey Mhando na mke wake, Eva Stephem Mhando, na maofisa wengine watatu wa shirika hilo, France Lucas Mcharange, Sophia Athanas Misidai na Naftali Luhwano Kisinga,  leo wamepandishwa kizimbani Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuhujumu uchumi na kuiingizia serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 884,550,000. 
 
Katika kesi hiyo iliyosomwa na Wakili wa Serikali, Leonard Swai, mbele ya Hakimu Frank Mushi, wakili huyo alisema Mhando akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco anatuhumiwa  kumpa tenda mke wake ya kusambaza vifaa vya stationery vyenye thamani ya shilingi milioni 884,550,000/ kwa shirika hilo kinyume na taratibu.
 Waliounganishwa kwenye kesi hiyo nao wakishuka kizimbani chini ya ulinzi mkali.
 Mke wa Mhando (kushoto) na mwenzake wakirudishwa mahabusu.
 Askari kanzu akitanua njia wakati Mhando (mwenye shati jeupe) akipelekwa kizimbani.

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment