WANADAMU wanazidi kuegemea kwenye imani utata! Hivi
karibuni, watu mbalimbali wenye magonjwa wamekuwa wakimiminika nchini
Nigeria na kuoga maji ya bwawa yanayodaiwa yanaponya magonjwa papo hapo.
Watu hao wakiwemo wazee, vijana waume kwa wake na wenye magonjwa
mbalimbali wamekuwa wakizama kwenye maji hayo kwa urefu wa futi tatu
hadi nne, wengi wakiwa uchi au nguo za ndani tu.
Wengine huchota maji hayo na kuosha sehemu yenye tatizo hasa wale wenye
kushindwa kuona au wenye vidonda sugu kama vile kansa, Ukimwi
nakadhalika.
Tangu kugunduliwa kwa bwawa hilo, zaidi ya watu 3000 wameshafika kuyaoga maji hayo kuanzia asubuhi hadi saa 12 jioni.
Hata hivyo, hakuna taarifa za moja kwa moja na uwazi kwamba watu wamepokea uponyaji.
Nigeria ni nchi yenye matukio mengi ya kiimani licha ya mambo ya kisiasa ambapo mpaka sasa wananchi wake wamekuwa wakikumbana nayo.
Baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakiwaambia waumini wao kuamini zaidi katika uponyaji wa Mungu.
Nchini Tanzania, miaka ya karibuni aliibuka Mchungaji Ambilikile Masapile ‘Babu wa Samunge’ akidai ana maji ambayo mtu mgonjwa akinywa anapata uponyaji.
Watanzania wengi, wakiwemo viongozi wa serikali walimiminika kwenye Kijiji cha Samunge, Loliondo kunywa kikombe chenye maji hayo lakini baadaye ilikuja kubainika kwamba, hakukuwa na uponyaji wowote zaidi ya kumwachia babu huyo utajiri.
0 comments:
Post a Comment