banner

Monday, May 5, 2014

Miongoni mwa stori zilizobamba wikiendi hii ni hii ya huyu mamba mkubwa kuuawa kwa risasi nne Kinondoni Dar


Miongoni mwa stori za mjini  zilizobamba wikiendi  hii ni hii ya Mamba kuuawa Block 41 Kinondoni Dar es salaam kwenye eneo  ambalo wanaishi watu kadhaa maarufu wa Tanzania akiwemo Kalapina wa kikosi cha Mizinga, hii ni nyuma ya bestbite, Mamba huyu akiwa ametokea kwenye bwawa  nyuma ya 41 Records.

Bwawa limezungukwa na nyumba kwenye eneo la kwa Kisamo zamani Kajima ambapo kwenye hili bwawa zamani kidogo kulikua na Mamba wawili ila baada ya kugundulika mmoja alichukuliwa na watu wa Wanyama ila mwingine hakuonekana.


  

Tukio la juzi ilikua saa nane usiku ambapo mamba huyu alijitokeza barabarani mtaani ndipo majirani wakamuita mtu  mwenye bunduki kwenye huo mtaa ili amuue kwa sababu mwanzoni kabla hawajajua walikua wanahofia kumuua wakidhani ni kosa la kisheria.

Baada ya kuuwawa kwa  risasi  nne, Defender ya Polisi ilikuja  na  kumchukua  huyu Mamba

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment