
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na Naibu wake Juma Nkamia wakiwa wameshikilia kombe la ushindi la Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) baada ya timu hiyo kutembelea Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara wakiwa wameshikilia Kombe la Dunia la Ushindi wa Mashindano ya Watoto wa Mitaani leo mjini Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba

Mkurugenzi wa Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC), Mutani Yangwe akisalimiana na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi mjini Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangar(kushoto) na Waziri wa Ardhi, Nyumbana Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka wa pili (kulia) wakiwa pamoja na timu hiyo.
Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) ikiwa katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya timu hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba leo
***
Na Magreth Kinabo/ MAELEZO –Dodoma
Mfungaji bora wa Timu ya Watoto wa Mitaani kutoka Mwanza Tanzania, (TSC)ambayo iliibuka mshindi katika mashindano Kombe la Dunia la Watoto hao yaliyofanyika Brazil, mwaka huu Frank William ameishauri , Serikali na jamii kuwasaidia watoto wa mitaani ili kuweza kukuza vipaji vyao.
Kauli hiyo ilitolewa leo mjini Dodoma na William wakati walipolitembelea Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma , wakiwa na viongozi wao ,ambapo walipata nafasi ya kuzungumza na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na Naibu wake Juma Nkamia.
Alisema siri ya ushindi wetu ni ushirikiano na kujituma, tukilikwenda kuwakilisha watoto wengine wa mitaani. Hivyo aliomba jamii kuwasaidia watoto wengi wa mitaani ambao hawana uwezo wa kupata elimu lakini wana vipaji mbalimbali ili waweze kuvikuza.
Kwa upande wake kipa bora wa timu hiyo, Emmanue Amos, alishauri Serikal iweze kuwasaidia ili waweze kushiriki katika mashindano ya mwaka 2018 ya kombe hilo.
Mchezaji mwingine wa timu hiyo ,Denis David aishauri jamii isiwadharau kwa kuwa ni watoto wa mitaani kwani wanavipaji wakipata watu wa kuwasaidia, hivyo aliitaka iwekeze katika soka la vijana kwa sababu baada ya miaka 20 ijayo mchezaji bora anapatikana kwa njia hiyo.
Aliwaomba wajumbe wa Bunge hilo ,kuwasaidia ili waweze kuvikuza vipaji vyao.
Naye Kocha wa timu hiyo,Suileiman Jabir alisema wadau mbalimbali kuwasaidia na kuwaendeleza watoto hao I, ambao ni wengi ambao wanaweza kuwa na vipaji vya sanaa na utamaduni.
Akizungumzia kuhusu mafanikio ya ushindi huo, ni kuwa na mpango wa kutafuta vijana wenye vipaji ambapo wanaviendeleza na kuvikuza kwa kufanya maandalizi ya kiutalaamu na kiufundi.
Jabir aliongeza kuwa waliwandaa kisaikolojia ili waweze kushinda katika mashindano hayo ya kimataifa.
Aliwataka wajumbe wa Bunge hilo, kuhakikisha saula la watoto hao, linapewa kipaumbele na kuweka sheria itakayowadhibiti wakina baba wanatekeleza watoto,huku akiisa jamii kuwasaidia watoto pale wazazi au walezi wanapofariki dunia.
Rais wa timu hiyo, Altaf Hirani aliiomba Serikali kuweza kuwasaidia kupata kiwanja cha michezo kwa ajili ya watoto jijini Mwanza au kwenye maeneo mengine ya nchi.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Michezo na Utamaduni akizungumzia kuhusu timu hiyo alisema ameliagiza Shirikisho la Mchezo wa Soka Tanzania (TFF) kuwa na mpango endelevu wa kuwasaidia watoto ili waweze kulisaidia taifa.
Timu hiyo iliibuka mshindi baada ya kuifunga Timu ya Burundi magoli 3-0.
0 comments:
Post a Comment