MABADILIKO YA UELEKEO WA BARABARA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZIA SIKU YA TAREHE 28/04/2014. (TRAFFIC CIRCULATION AT CBD)
Ufunguo wa ramani iliyopachikwa hapo juu:-
- RANGI YA NJANO - Njia ya uelekeo mmoja (One Way)
- RANGI YA BLUE MPAUKO - Njia ya mielekeo miwili (Two Way)
- RANGI YA KIJANI - Mitaa ya kutembea kwa miguu, magari marufuku (Walking streets)
- RANGI NYEKUNDU - Barabara za kupita daladala
- RANGI YA BLUU ILIYOIVA - Barabara za DART
- DUARA ZA NJANO - Mzunguuko (Round-about)
- MSALABA WA KIJANI - Makutano yenye taa za kuongozea Magari (Signalized intersection)
1. Kipande cha Mtaa wa Samora kuanzia Mnara wa Askari (Askari Monument) hadi Clock Tower. Magari kutakuwa na mabadiliko ambayo magari yatakuwa yanaelekea Clock Tower badala ya Askari Monument.
2. Barabara ya Sokoine kuanzia Station hadi makutano ya Mtaa wa Maktaba, Posta ya Zamani, magari yatakuwa yanaelekea Uelekeo mmoja wa Station, Posta ya Zamani tofauti na ilivyo sasa Posta ya Zamani kwenda Station.
3. Barabara ya Kivukoni kuanzia Posta ya Zamani hadi ferry itakuwa barabara ya mielekeo miwili (Two Ways).
4. Barabara ya Samora kuanzia mnara wa Askari hadi Ocean Road Hospital itakuwa ni barabara ya mielekeo miwili.
5. Daladala zote zitakazotokea barabara za Makataba zitakunja kulia pembeni ya jengo la NBC na hadi makutano ya Mkwepu na kukunja kushito kuingia Sokoine pale Posta ya Zamani na baadaye kukunja kushoto kuingia Makataba na kurudi Posta Mpya.
Kwa Maelezo zaidi Wasiliana na Ofisi za DART zilizopo UBUNGO PLAZA GHOROFA YA KWANZA au kwenye OFISI YA MHANDISI WA MANISPAA YA ILALA, mkabala na SHOPRITE SUPERMARKET, jirani na KAMATA.
Mtaarifu mwingine juu ya mabadiliko haya kuondoa usumbufu ifikapo siku ya Jumatatu 28/04/2014.
0 comments:
Post a Comment