banner

Friday, April 25, 2014

Rais Kikwete amtolea uvivu Dr. Mwakyembe.....Ni kuhusu upitishaji dawa za kulevya Airport, atoa mwezi mmoja....Aahidi kutimua watendaji





RAIS Jakaya Kikwete amesema anaumia, kuchukizwa sana anapoona Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam (JNIA) na Kilimanjaro (KIA), vinapokuwa uchochoro wa kusafirisha dawa za kulevya kwenda mataifa mbalimbali.

Kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete ametoa mwezi mmoja kwa Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe na watendaji wake akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwaja vya Ndege nchini, Mhandisi Suleiman Suleman, kudhibiti mianya yote inayotumika kupitisha dawa hizo katika viwanja hivyo.

Rais Kikwete aliyasema hayo Dar es Salam jana wakati akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa jengo jipya la JNIA na kusisitiza ujenzi huo ukikamilika utakuwa na manufaa kwa Taifa.

"Kitendo cha watu wanaofanya biashara ya dawa za kulevya kupita nchini kirahisi katika viwanja hivi na kwenda kukamatiwa nje ya nchi kinaniuma na kunikera sana...hii ni aibu kwenye Taifa hivyo nataka udhibiti uanze mara moja.

"Wafanyabiashara wa dawa hizi wanapita watakavyo, jengo hili likikamilika biashara hii inaweza kuwa huria...hii ni aibu sana ndio maana nasema inaniuma, huu ni uzembe mkubwa," alisema.

Aliongeza kuwa, utendaji wa Dkt. Mwakyembe unaweza kuingia doa kutokana na udhibiti mbovu wa kupitisha dawa za kulevya katika viwanja hivyo na kuwataka watendaji wake, wamsikilize Waziri huyo na kuyafanyia kazi maagizo anayotoa ambayo kimsingi yanatoka kwake hivyo wasipotekeleza ataanza kuwachukulia hatua watendaji husika akiwemo Mhandisi Seleman.

Rais Kikwete alisema kama tatizo hilo litadhibitiwa ipasavyo, atafurahi hivyo jambo la msingi ni watendaji husika kubana mianya yote inayopitisha dawa hizo katika viwanja hivyo na wale ambao watakwamisha utekelezaji, apelekewe majina yao ili awaondoe.

"Suala la kuwaondoa watendaji ambao itabainika wanahusika na biashara ya dawa za kulevya halinishindi na hakuna wa kunishtaki, Rais ashtakiwi hivyo msimuonee haya mfanyabiashara yeyote anayefanya biashara hii ambayo ni haramu," alisema.

Alisema atahakikisha hazina inatoa pesa za mradi huo kwani ujenzi huo ni ishara ya kufikia malengo ya kukua kiuchumi ifikapo 2015 ambapo sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii itakuwa na kutaka ieleweke wazi kuwa, viwanja vya ndege ndio lango kuu la nchi, kutoa taswira nchi na wananchi wake jinsi walivyo.

Kwa upande wake, Bw. Mhandisi Suleman alisema ujenzi wa uwanja huo umeanza Januari mwaka huu, unatarajia kukamilika Oktoba 25,2015 na utagharimu sh. bilioni 518 ambazo ni mkopo kutoka Benki ya HSBC ya Uingereza kwa dhamana ya Serikali ya Uholanzi.

"Jengo hili linajengwa mita za mraba 70000m2, litakuwa na miundombinu yake ikiwemo uwezo wa kuhudumia abiria milioni sita, mifumo ya mawasiliano, usalama, uendeshaji, maegesho ya ndege na viungio vyenye uwezo wa kuegesha ndege aina zote kubwa za kisasa duniani

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment