Basi aina ya Urio yenye namba za usajili T 137 BCX inayofanya safari zake moshi kuelekea leguruki mkoani Arusha jana jioni limepinduka katika eneo la KIA na kujeruhi watu zaidi ya 31.Mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio walisema kuwa dereva huyo alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki iliyokuwa imejichomeka barabarani.
"Dereva alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki ndipo gari ikamshinda na kuhama barabara , ikaanguka na kubiringika mara tatu kichwa chini matairi juu" alisema mmoja wa shuhuda ambaye akutaka kutaja jina
0 comments:
Post a Comment