Mkongwe wa Dansi nchini, Maalim Muhidin Gurumo aliyekuwa akitumikia Bendi ya Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ kabla ya kustaafu mwaka jana, amefariki dunia.
Mwanamuziki huyo amefariki leo alasiri katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Mzee Gurumo amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu, hali iliyomfanya astaafu muziki....
Msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata Makuburi na mipango yote ya mazishi itafanyika hapo.....
Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi-Amina
0 comments:
Post a Comment