MAMA MZAZI WA MTOTO ALIYEIBIWA
BABA MZAZI ANAYETUHUMIWA KWA WIZI WA MTOTO
Jeshi
la Polisi linamshikilia Salehe Issah Mwangosi(29) Mkazi wa Tankini
Kasumulu Kata ya Itope Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya kwa tuhuma za wizi
wa mtoto jinsi ya kiume mwenye umri wa siku sita.
Imedaiwa kutenda kosa hilo dhidi ya mzazi mwenzake
aliyefahamika kwa jina la Mboka Mwakikagile(21)mkazi wa Kitongoji cha
Sama A Kijiji cha Ibanda Kata ya Itope Jumapili April 6 mwaka huu majira
ya saa nne asubuhi kwa kushirikiana na mwanamke mmoja ambaye
hajafahamika jina mara moja aliyejifanya ni mama yake mkubwa wa
mtuhumiwa.
Mipango hiyo iliyoanza kuandaliwa na mtuhumiwa siku
tatu baada ya mtoto kuzaliwa kwa kutumia simu ya kiganjani ya mtuhumiwa
yenye namba 0767356222 na mzazi wa mtoto kwa namba 0757006839 ambapo
siku ya tukio Salehe alimwambia kuwa mama yake mkubwa angekwenda
kumjulia hali mtoto aliyezaliwa.
Baada ya Salehe kuwasiliana na mzazi mwenzake
walikubaliana Mama yake mkubwa angekwenda Jumapili Aprili 6 mwaka huu
majira ya saa nne asubuhi ambapo mwanamke huyo alifika nyumbani kwa
Mboka(Mzazi wa mtoto)ambapo aliwakuta wazazi wake akiwemo Mzee Lupalo
Elija Mwakikagile(90) na mkewe Nelly Kyusa(49) ambao walimpokea.
Mwanamke huyo alifikanyumbani kwa Mwakikagile akiwa
ameshika mkoba wenye nguo za mtoto mchanga,sabuni na mahitaji mengine
ambapo alijieleza kuwa yeye ni afisa wa Mamlaka ya mapato na Mama mkubwa
wa Salehe hivyo amekuja kwa ajili ya kumjulia hali na kumpa pole Mboka
kwa kujifungua.
0 comments:
Post a Comment