banner

Saturday, April 12, 2014

Mtuhumiwa Sugu wa Ujangili auawa kwa kupingwa Risasi ya mgongo na Polisi mkoani Simiyu


  Polisi mkoani Simiyu kwa kushirikiana na askari wa Idara ya Wanyamapori katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, wamemuua jangili sugu Majadiga Makabajinga au Mashaka Sai, kwa kumchapa risasi ya mgongo.

Sai, ambaye alikuwa akisakwa kwa muda mrefu, anatuhumiwa kuwa kinara wa ujangili na aliuawa wakati akipambana na polisi alipojaribu kuwatoroka baada ya kutiwa mbaroni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo, alisema Sai aliuawa juzi saa 3:00 usiku katika kijiji cha Mwasinansi wilayani Bariadi.

Alisema mtuhumiwa huyo alitiwa mbaroni na baada ya kuhojiwa alikiri kuhusika kwenye matukio mbalimbali ya ujangili pamoja na kifo cha askari wa wanyamapori.

Mbali na kuhusika kwenye matukio hayo, Sai alikuwa akiwafanyia ukatili ikiwa ni pamoja na kuwaua raia aliowahisi wanatoa taarifa zake kwa vyombo vya usalama.

Alibanwa na kukiri kuhusika na ujangili na siku nyingi tulikuwa tunamsaka. Ndiye alihusika na mauaji ya faru katika Hifadhi ya Serengeti (Mama Serengeti), alisema Kamanda Mkombo.

Hata hivyo, alisema baada ya mahojiano hayo, askari walimtaka awapeleke mahali anapohifadhi silaha, ndipo alipowapeleka katika kijiji cha Mwasinasi, ambapo awalionyesha sehemu ya kichaka.

Wakati askari wakifanya upekuzi kutoa silaha hizo, Sai alichukua mti na kumshambulia askari wa wanyamapori Christian Mlema kichwani kisha kumpora silaha na kuanza kufyatua risasi hewani.

Polisi walianza kujibu na kufanikiwa kumpiga risasi mgongoni na kudondoka.

Katika kichaka hicho, polisi walikuta bunduki mbili SMG iliyokuwa na magazine mbili na SR moja, zote zikiwa na risasi 50 pamoja na meno ya tembo.


Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment