banner

Wednesday, April 16, 2014

Mafuriko jijini Dar...... Idadi ya waliofariki 41


Mafuriko  yaliyotokea Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki yamesababisha vifo vya watu 41.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema vifo 25 vimethibitishwa. Ameagiza polisi kufanya uchunguzi zaidi kubaini watu wengine ambao hadi sasa hawaonekani waliko.

Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, eneo la Ilala, vilitokea vifo 11 ingawa inahisiwa watu wengine wawili hawaonekani. Kinondoni vifo ni saba huku wengine 14 wakidaiwa kuzikwa bila polisi kupata taarifa na Temeke vifo saba.

Sadiki alitaka uchunguzi wa polisi ufanyike kila familia zilizokumbwa na msiba, hususani Kinondoni kuthibitisha kama vifo hivyo 14 vilitokana na mafuriko.

Kuhusu kurudi katika makazi yao kwa wakazi wa Jangwani alitaka watumie busara kwani kitendo hicho kinahatarisha maisha yao.

Alisema serikali haiwezi kubomoa nyumba husika kwani inasubiri uamuzi wa mahakama kutokana na kuwepo kwa kesi iliyofunguliwa dhidi yake



Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment