Ni visa mbavyo wengi tulivisikia katika hadithi za kale, watu kuliwa na majitu, lakini katika siku za karibuni tumeshuhudia watu wakila viungo vya wenzao Jamhuri ya Afrika ya Kati katika jazba ya kulipiza kisasi dhidi ya watu waliowadhulumu katika uongozi uliong'olewa mamlakani wa Seleka.
Nchini Pakistan Polisi wamewakamata wanaume wawili kwa makosa ya kuiba maiti ya mtoto kutoka kaburini na kisha kumla.
Wawili hao Arif Ali na kakake Mohammed Farman Ali waliachiwa huru baada ya kuwa jela kwa miaka miwili kwa kula nyama ya binadamu.
Hata hivyo wawili hao wameonekana kuwa na tamaa kubwa ya mchuzi wa nyama ya binadamu.Wakaazi hao wa kijiji cha Daryabn Khan jimbo la Punjab walikamatwa mwaka 2011.
Polisi walisema kwamba walipata kiwiliwili cha maiti ya msichana mdogo kikiwa bila miguu na mikono.Wawili hao walikiri kwamba walipika mchuzi wa nyama ya viungo hivyo na kuvila.
Walishtakiwa kwa makosa ya kuharibu kaburi kwani nchini Pakistan hakuna sheria inayozungumzia hatia ya mtu kumla mwenzie.
Punde baada ya kuachiwa Arif Ali aliambia BBC kwamba anajutia makosa hayo na kwamba hatarudia tena.
Hata hivyo punde si punde polisi wamesema waliitwa na majirani wa jamaa huyo wakilalamikia uvundo mkali kutoka kwa nyumba yake.
Walipoingia chumbani humo Lo ! wakapata kichwa cha mtoto.Kiwiliwili hakijulikani kililiwa au kapotelea wapi. Arif Ali tena amekamatwa kwa mara ya pili na polisi wanaendelea kumsaka kakake.
Polisi wanaamini ndugu hawa walifukua maiti ya mtoto ambaye kichwa kilipatikana ndani ya makaazi yao.Arif anamlaumu kakake Farman.Wawili hao waliwahi kuoa na hata wakajaliwa watoto, hata hivyo wake zao waliwatoroka kabla ya kukamatwa kwao na kufungwa jela kwa kisa cha awali.
SOURCE: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment