Umoja wa katiba ya wananchi ( UKAWA ) , juzi wamepokelewa kwa mabango katika wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu yaliyowataka warudi bungeni kabla ya kuanza mkutano wao kwenye uwanja wa michezo wa Halmashauri ya mji huo ambao ulihudhuriwa na watu wachache.....
Mabango hayo yalikuwa na ujumbe uliowataka wajumbe wa umoja huo kurudi bungeni kujadili rasimu ya pili ya katiba ili kushindana kwa hoja na wajumbe wa bunge hilo weye mtazamo tofauti na wao....
Ujumbe wa Umoja huo ulioongozwa na mwenyekiti wa vijana chama cha demokrasia na maendeleo ( BAVICHA ) taifa, Bw. John Heche ulishangaa kuona mabango hayo na mahudhurio ambayo hawakuyatarajia licha ya mkutano huo kutangazwa siku mbili katika mji mzima....
Wakiwa wamebeba mabango hayo, wananchi hao waliutaka ujumbe huo kuwashawishi wajumbe waliosusia vikao vya bunge warudi bungeni ili kujadili matatizo ya watanzania na si muundo wa serikali....
"Sisi hatuna haja na muundo wa serikali hata zikiwa 10 , mbili au 3, tunataka kunufaika na pamba,bei iongezeke, tupate pembejeo za kutosha na kupewa matrekta ili tuweze kunufaika," alisema Bw. Mugata Munghu.
Wakazi wengine walioshiriki mkutano huo walidai asilimia kubwa ya wakazi wa mkoa huo ni wakulima na wafugaji ambapo changamoto kubwa waliyo nayo ni ukosefu wa maeneo ya kufanyia uzalishaji....
"Hatuna maeneo ya kulishia mifugo yetu na kufanya shughuli za kilimo,rudini bungeni mkatutetee tupate maeneo ya kutosha kwa ajili ya wafugaji na wakulima, tunataka kuachana na mapigano ya kila siku, wekeni sheria ya kuilazimisha serikali itenge maeneo haya, hatuoni umuhimu wa nyie kutanga taga nchi nzima kutaka serikali tatu," alisema Bw. John Matale
Viongozi wa umoja huo waliendelea kuhutubia mkutano huo mbali ya kuwepo kelele za vijana waliokuwa wakizunguka na mabango huku viongozi hao wa UKAWA wakitumia muda mwingi kumshambulia katibu mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana.
0 comments:
Post a Comment