Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alisema tukio hilo lilibainika Mei 20 mwaka huu majira ya saa 4:45 Asubuhi katika eneo la mtaa Azimio kata ya Kiwanje Ndege Morogoro.
Alisema majirani walizingira
nyumba ya mwanamke ajulikanae kwa jina la Maria Said na kutaka kuvunja
ndipo polisi walipopata tarifa na kufika katika nyumba hiyo na kukuta
mtoto huyo akiwa katika box.
Alimtaja mtoto huyo
aliyejulikana kwa jina la Nasra Rashid Mvungi mine na nusu ambapo
polisi ilichukua jukumu la kupeleka kesi hiyo Ustawi wa jamii ili
kuendela nayo.
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul
Maria Said mama mkubwa wa
Nasra, katikati ni baba mzazi wa Nasra, Rashidi Mvungi, na kulia ni mume
wa Mariam Said wakiwa katika ofisi za ustwawi wa jamii mjini Morogoro
Afisa Ustawi wa jamii katika
ofisi ya mkoa wa Morogoro Oswing Ngungamtitu alisema mtoto huyo
alipelekwa hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa sababu alionekana
kuwa na afya dhoofu.
Alisema alilazwa na kwamba kwa
sasa yupo chini ya uangalizi wa ustawi wa jamii huku wakiwachukulia
hatua za kisheria walezi wa mtoto huyo Mariam Said na Mume wake Mtonga
Omari.
Baba mzazi wa mtoto huyo
alisema yeye ana mke na watato wengine wa ndoa na kwamba hakuwahi
kumwambia mkewe kama ana mtoto wa nje hivyo ilikuwa vigumu kumchukua
mtoto huyo na ndipo alipomkabidhi mama mkubwa wa mtoto huyo.
Alisema kila mara alikuwa
akifika kumwona mtoto mama huyo alimwambia mtoto kalala na hivyo
kushindwa kumwona na kujua hali halisi hadi siku ya tukio na kwamba
alikuwa akimpatia matumizi ya mtoto huyo.
Ofisa mtendaji wa kata hiyo Dia
Zongo alisema akiwa katika kazi za kawaida katika Mtaa wa Azimio,
alipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mwanamke huyo, alimficha mtoto
Nasra ndani ya boksi na kwamba hamfanyii usafi wala kumtoa nje.
Zongo alisema baada ya kupata
taarifa hizo, alimtafuta Mwenyekiti wa mtaa huo, Tatu Mgagala na
kuongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo na kuanza kumhoji mwanamke huyo
ambaye alikuwa akijibu kwa kubabaika na kushindwa kueleza ukweli juu ya
kuwepo kwa mtoto huyo.
Zongo alisema wakati mtuhumiwa
akiendelea kujibu maswali, ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza
kukohoa hali iliyowapa wasiwasi na kuamua kuingia chumbani kwa mwanamke
huyo kwa nguvu na kumkuta mtoto Nasrah akiwa ndani ya boksi nyuma ya
mlango .
Ofisa mtendaji huyo alisema
wakati wakimtoa mtoto huyo kutoka ndani ya nyumba ya mama yake huyo
mkubwa, ghafla kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo na mawe, walianza
kumshambulia mwanamke huyo, kitendo kilichomlazimisha (mtendaji) kutoa
taarifa polisi.
Waburuzwa polisi
Baada ya kufikishwa katika kituo cha polisi mwanamke huyo alikiri kuanza kumlea mtoto huyo tangu akiwa akiwa na umri wa miezi tisa na kwamba hatua hiyo ilikuja baada ya mama yake, kufariki dunia mwaka 2010.
Mtuhumiwa huyo alisema kwa mara
ya mwisho, alimuogesha mtoto huyo Julai mwaka jana na kwamba alikuwa
akimwekea chakula na maji ndani ya boksi lililokuwa limewekwa nyuma ya
mlango wa chumba cha mwanamke huyo.
Hores Isaack Msaky Dk Mshauri wa watoto katika hospitali ya mkoa wa
Morogoro alikiri kumpokea mtoto huyo na kwamba tayari ameshaanzishiwa
matibabu ya awali .‘’ Tulimfanyia vipimo vya awali mtoto amebainika kuwa na Nimoni pamoja na utapia mlo na sasa ameshaanza matibabu’’ Alisema
Alisema bado wanaendela na vipimo vingine vya XRay kubaini mtoto huyo alipata ulemavu kwa kupigwa au alizaliwa hivyo.
Alisema mtoto huyo anamaumivu
makali sehemu ya mgongo na mikono na kwamba mwili wake pia ni mteke
kama wa mtoto mchanga hali inayowafanya kuendela kumfanyia uchunguzi wa
kina zaidi.
Baadi ya mashuhuda wa tukio
hilo walidai kuwa mama wa mtoto huyo alifariki dunia miaka mine iliopita
na kwamba Mariamu Ni mama mkubwa wa mtoto huyo.
Hata hivyo majirani hao
walidai wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikina kutokana na
kwamba mama huyo anaakili timamu na analea watoto wake vema tofauti na
mtoto huyo.
0 comments:
Post a Comment