banner

Wednesday, May 14, 2014

UKATILI! Kichanga cha Siku 2 chaokotwa kikiwa kimetupwa eneo la Mto Ng’ombe Jijini DAR..!


Kichanga kikiwa kimetupwa eneo la mto Ng’ombe Mwananyamala jijini Dar.


Wakazi wa Mwananyamala wakiwa eneo la mto Ng’ombe kushuhudia tukio hilo.
MWILI wa kichanga kinachokadiriwa kuwa na siku mbili umeokotwa ukiwa umetupwa eneo la mto Ng’ombe jirani na Rasco, Mwananyamala jijini Dar.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, kichanga hicho cha kiume kimekutwa eneo hilo leo asubuhi kikiwa kwenye mfuko wa Rambo.
Mtandao huu ulifanikiwa kuongea na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho, Bi. Husna aliyetoa rai kwa wananchi wa eneo lake kutojihusisha na vitendo viovu kama hiki, huku akiwasihi kutumia njia za uzazi wa mpango kujikinga na matatizo kama hayo.
“Nina masikitiko makubwa kwa kitendo hiki, ni bora kichanga hiki kingeletwa serikalini tukilee kuliko kutupwa eneo hili. Kama wananchi mkishindwa kuvumilia bora mtumie uzazi wa mpango,” alisema Bi. Husna huku akiahidi kufanya uchunguzi wa kina kumtafuta muhusika!

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment