banner

Thursday, May 15, 2014

Serikali yasema VIPIMO na MATIBABU ya homa ya Dengue ni BURE


 Magreth Kinabo – MAELEZO
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, amewataka wananchi wa mkoa huo wanapohisi wana dalili za ugonjwa wa dengue kuwenda katika hospitali za Serikali kwa kuwa matibabu hutolewa bila malipo.

Aliyasema hayo kwenye ukumbi wa mkutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuulizwa swali juu ya gharama kubwa za matibabu ya ugonjwa huo:

    “Tunaomba wananchi wanapohiisi dalili za ugonjwa huo kwenda katika hospitali za Serikali, ambazo ni Amana, Mwananyamala na Temeke kwa kuwa matibabu yanatolewa bila malipo.”


  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi,  Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja alisema vituo vyote vya Serikali vinapaswa kutoa matibabu ya ugonjwa huo bila malipo kwa kuwa ugonjwa huo ni mlipuko na magonjwa ya milipuko matibabu yake hutolewa bila malipo.

Mwamwaja pia alisema ikitokea hata vituo vya afya vya binafsi vikapewa vitenganishi na vifaaa vya tiba na Serikali navyo vinasapwa kutoa matibabu ya ugonjwa huo bila malipo.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa sasa wanajenga uwezo ili kila wilaya iwe na vituo vitano kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa huo.

Sadick aliongeza kuwa Serikali itanyunyuzia dawa ya (Larvicide) sehemu za mikusanyiko kama vile mashuleni na kwenye madimbwi, lakini maeneo ya hoteli na baa watapaswa kunyunyuzia dawa kwa gharama zao:

    “Kwa upande wa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, wanapaswa kunyunyuzia dawa kwa gharama zao, (yaani matumizi mengineyo)”
alisisitiza huku akisema hata kwenye Ofisi yake wamefanya hivyo kwa gharama zao.

Aidha Sadiki aliwataka viongozi wa mitaa na watendaji wengine kuwahimiza wananchi kuhusu usafi wa mazingira ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.

Alisema wananchi wanapaswa kuhakikisha vifuu vya nazi visoda kwani maji kidogo yanayokaa katika vitu husababisha mbu wanaosabbaisha ugonjwa huo kuzaliana , hivyo vinatakiwa visitupwe ovyo na kufunika maji safi wanayoyahifadhi.

Alisisitiza hatua ya kwanza kuzuia ugonjwa huo ni usafi wa mazingira, hivyo dawa ni hatua ya mwisho.

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment