banner

Thursday, May 8, 2014

Majanga! Mtanzania mwingine akamatwa Airport Nairobi akiwa na mzigo wa dawa za kulevya….

dawa

Mwanaume mmoja Mtanzania amekamwata katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi Kenya akiwa amebeba dawa za kulevya akiwa njiani kuelekea Antananarivo ambapo mzigo huo ulitokea Tanga kisha ukapita Mombasa na baadae kwa ndege mpaka Nairobi.
Mzigo wenyewe ni wa cocaine na Heroin ambazo zote zina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 24 za Kitanzania na dawa hizo alikua  ameziingiza katika njia ya haja kubwa.

Mkuu wa kitengo cha CID katika uwanja huo Joseph Ngisa amesema mshukiwa alikamatwa JKIA na akawekwa kwenye chumba cha uchunguzi na baadae akatoa tembe za cocain na tembe za Heroin na tayari ameshapelekwa Mahakamani.
Mwezi March mwaka huu watanzania wanne walikamatwa katika uwanja huohuo walipopatikana na heroin yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 75 za Kitanzania na wote walifikishwa mahakamani na kukiri kosa.
Wanawake watatu na mwanaume mmoja kila mmoja akishtakiwa kando kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya na walikua wameingia Kenya kupitia Namanga na walikamtwa wakiwa njiani kuelekea Hong Kong.

dawa2

Kuanzia March 2014 mpaka leo hii May ni jumla ya Watanzania watano wamekamatwa kwenye kiwanja cha ndege Nairobi wakiwa kwenye pilika za kusafirisha dawa za kulevya kwenda kwenye mataifa mengine.

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment