banner

Friday, May 23, 2014

Maalim Seif kugombea tena Ukatibu Mkuu CUF, Achukua Fomu leo


 Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akichukua fomu ya kugombea tena nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho katika ofisi kuu za CUF Wilaya ya Magharibi Kilimahewa Zanzibar. Anayemkabidhi ni Kaimu Katibu wa CUF Wilaya ya Magharibi Ussi Juma Hassan.
 
 
 Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha fomu ya kugombea tena nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho katika ofisi kuu za CUF Wilaya ya Magharibi Kilimahewa Zanzibar.
 
 
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wanachama waliojitokeza kumsindikiza wakati wa kuchukua fomu hiyo. katika ofisi kuu za CUF Wilaya ya Magharibi Kilimahewa Zanzibar.


Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na waandashi wa habari katika ofisi kuu za CUF Wilaya ya Magharibi Kilimahewa Zanzibar, baada ya kuchukua fomu ya kugombea tena nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho (Picha na Salmin Said, OMKR)
 
Na Hassan Hamad OMKR
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo amechukua fomu ya kugombea tena nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho.
 
Maalim Seif amechukua fomu hiyo katika Ofisi za CUF zilizopo Kilimahewa Wilaya ya Magharibi Unguja, na kusindikizwa na viongozi na wanachama kadhaa wakati akichukua fomu hiyo.
 
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu hiyo Mhe. Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema ameamua kuchukua fomu hiyo ili aendelee kuwatumikia wanachama na kufikia malengo ya chama waliyojiwekea.
 
Amefahamisha kuwa pia ameshawishika kuchukua fomu hiyo baada ya kujitokeza kauli za kutaka kuzorotesha serikali ya umoja wa kitaifa.
Amesema akiwa kiongozi wa Chama ataendelea kuwatumikia wanachama na wananchi hadi pale chama kitakapotimiza malengo yake

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment