SERIKALI ya Kenya imethibitisha kuwa maofisa wake
wawili wa jeshi wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa, baada ya
wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shaabab kufanya shambulio la kuvizia, baada
ya magari yao kukwama barabarani huko Somalia.
Ripoti zinasema msafara wa wanajeshi wa Kenya ulikuwa ukielekea eneo
la Ras Kamboni wakati shambulio hilo lilipotokea. Kamanda wa polisi
mjini Mombasa, Robert Kitur amethibitisha kuwa shambulio hilo limetokea.
Kwa upande wao, msemaji wa Al shabaab, Abu Mus’ab amedai kuwa
wapiganaji wake walifanikiwa kuteketeza magari kadhaa ya Jeshi la Kenya,
madai ambayo yamekanushwa vikali na utawala wa nchi ya Kenya.
Monday, May 26, 2014
Al Shabaab waua Wanajeshi wawili wa Kenya Somalia.
Unknown
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment