Meya wa jiji la Dar es Salaam,Dr Didas Massaburi amesema abiria wataokutwa wakiwa wamepanda Pikipiki maarufu kama Boda boda katika maeneo ambayo pikipiki hizo hazina leseni ya kufanya biashara watakamatwa na kufikishwa mahakamani pamoja na dereva.....
Alisema pia wafanyabiashara wadogo wataokutwa wakifanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria ikiwemo maeneo ambayo yamefanyiwa usafi na Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam hivi karibuni watakamatwa na kufikishwa mahakamani.....
Meya huyo aliyasema hayo jijini Tanga hivi karibuni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambao walitaka kufahamu msimamo wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania ( ALAT ) kuhusu kunyanyaswa kwa waendesha bodaboda katika maeneo mbalimbali nchini
0 comments:
Post a Comment