
Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imetwaa ubingwa wa
Dunia wa Watoto wa Mitaani baada ya kuilaza Burundi mabao 3-1 katika
mchezo wa fainali uliochezwa jana (Aprili 6), jijini Rio de Janeiro,
Brazil.
Mshambuliaji Frank William alifunga mabao matatu katika mechi hiyo
iliyochezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense huku mgeni
rasmi akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza, George Osborne.
Tanzania ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuitandika
Marekani mabao 6-1 ambapo hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 4-0.
Burundi ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika mechi ya nusu fainali ya pili.
Timu ya Tanzania inarejea nchini Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu)
ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa
10 jioni kwa ndege ya Emirates.
0 comments:
Post a Comment