banner

Friday, April 18, 2014

Telex free yawaliza watanzania; mamilioni ya fedha yateketea!

Baada ya muda mrefu tangu tahadhari zitolewe kuhusu wale waliojiunga na mtandao wa Telex free kuwa ni "illegal" na Benki Kuu ya Tanzania haitambui mtandao huo wa "online marketing", sasa yametimia maana mtandao wa Telex Free UMEFUNGWA rasmi.

Watanzania zaidi ya 20,000 wadaiwa kupata hasara kubwa ya kifedha na mpaka sasa hawajui namna ya kukomboa fedha zao.

Itakumbukwa kuwa ili uweze kufungua "account" Telex Free ni lazima ulipie kiingilio ambacho kilikuwa kinaanzia 600,000 TZS na kuendelea. Hivyo, hatua ya kufungwa kwa mtandao huo kumepoteza fedha zote za kiingilio na faida zote ambazo wanachama wa Telex Free walijipatia pindi walipokuwa wakifanya kazi na mtandao huo.
 

Poleni sana Watanzania wenzangu mliopatwa na janga hili. Hakika Pasaka imekuja vibaya sana.

Socializer Widget By Blogger Yard
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →

0 comments:

Post a Comment