Nchini Kenya Julius Kipkoitch anaripoti kwamba wakazi wa jiji la Eldoret wamemfanya kila
alieiona hii kuvutiwa na pengine kujua imekuaje wakafanya hivi kwa mara
ya kwanza baada ya kujitosa na kupiga deki barabara ya lami ya Oginga
Odinga jijini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya.
Unaambiwa wameamua kufanya hivi ikiwa ni maandalizi ya kumlaki nabii
Daktari Awuor kwa ajili ya maombi ya leo na siku ya Jumatatu kuadhimisha pasaka na kumshukuru jehova kwa kuwasaidia jiji la Eldoret kufanyika uchaguzi wa amani mwaka 2013
Hata hivyo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii maoni yalikotolewa na Wakenya kuhusu hii
ishu, maoni mengi yameonekana kupinga kitendo cha waumini hao wa kanisa
la Jesus is lord kwa kumpa Daktari Awuor heshima kupita kiasi.
Mkurugenzi mkuu wa Kass media inayo miliki Radio ya kass fm
inayotangaza kwa lugha ya kikalenjin inayozungumzwa na wakazi wa jiji la
Eldoret Julius
lamaon, amesema ‘watu wetu waache kupotoka, jiji letu limebadilishwa na
kuwa jiji la vituko…… Gavana hatakiwi kuhudhuria mkutano huu’
0 comments:
Post a Comment