Hali bado si shwari katika kampuni ya ujenzi wa barabara ya magari yaendayo kasi ‘STRABAG’ iliyopo maeneo ya Ubungo jijini Dar, ambapo asubuhi hii Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wametanda eneo la ofisi hizo na hakuna mfanyakazi yeyote wa kawaida anayeruhusiwa kuingia ndani.
Mgomo huo ulioanza Jumatatu, Aprili 28 mwaka huu leo ulikuwa unaingia siku ya tatu ambapo wafanyakazi wanapinga uongozi wa kampuni hiyo kuwalipa mishahara midogo, kuwaondolea posho zao za wiki na suala la kutopewa ajira kwa vibarua waliofanya kazi kwa muda mrefu katika kampuni hiyo.
0 comments:
Post a Comment