Halmashauri
ya Wilaya ya Kilombero imeamua kufuta miliki ya mashamba yote makubwa
yasiyoendelezwa na taratibu mpya zinafanyika ili kuyamilikisha kwa
wananchi.
Kati ya mashamba hayo, matatu ni ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
marehemu Daudi Balali na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Klabu ya Simba,
Marehemu Priva Mtema yaliyoko katika vijiji vya Lungungole na Merera
ambayo wananchi wameshayavamia na kuendeleza shughuli za kilimo.
Akizungumza
katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Kilombero juzi,
Mwenyekiti wake, David Ligazio alisema taratibu za kuomba hatimiliki za
mashamba hayo zifutwe zinaendelea.
Ligazio
alisema wamiliki wa mashamba hayo wameshapewa notisi na orodha yao
imeshawasilishwa kwa Kamishna wa Ardhi ili aridhie kufutwa kwa hati za
mashamba hayo.
Alisema
uamuzi wa kuyataifisha umekuja baada ya halmashauri kubaini kuwa
yamekuwa hayaendelezwi na hivyo kusababisha maeneo hayo kuwa misitu
wakati wananchi wanahitaji maeneo ya kulima.
Alisema
ukaguzi wa kumbukumbu umeonyesha kuwa idadi kubwa ya wamiliki hao
hawapo wilayani Kilombero na maeneo hayo yanamilikiwa kwa hati za muda
mrefu bila kufuata taratibu.
Alisema
utaratibu unaofanyika sasa ni kuwaagiza watendaji na wenyeviti wa
vijiji, kuanisha ukubwa halisi wa mashamba hayo ili kurahisisha kazi ya
kuyagawa kwa wananchi katika siku zijazo.
Akizungumzia
hatua hiyo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa
Anna Tibaijuka alisema taarifa hiyo haijafika ofisini kwake, lakini
akabainisha kuwa kuna watu wengi wanaomiliki ardhi kubwa mkoani Morogoro
bila kuwa na hatimiliki wala kufuata taratibu huku wakiwa wanawatisha
wananchi.
Aliwataka
wananchi hao kujisimamia, waondoe unyonge na kuzingatia taratibu za
ardhi, kwamba inatakiwa kugawiwa kupitia mkutano mkuu wa kijiji,
vinginevyo wana haki ya kujitwalia maeneo hayo na kufanya maendeleo
mengine.
“Kuna
matukio unakuta mtu anakaa na mwenyekiti wa kijiji na kujifungia,
wanajadili wenyewe na kugawiana maeneo ya kijiji bila kuwashirikisha
wananchi, hawa wananchi wanatakiwa kukataa hali hiyo,” alisema.
Maeneo yanayogawiwa
Mwenyekiti
wa halmashauri aliyataja maeneo mashamba yanayotakiwa kugawanywa kwa
wananchi na ukubwa wake katika mabano kuwa ni Lungongole (ekari 375) na
Merea (ekari 373). Pia kuna shamba lenye ukubwa wa hekta 887
linalomilikiwa na Balali, ekari 491 zinazomilikiwa na George Teni katika
Kijiji cha Kisegese na ekari 500 zinazomilikiwa na Aloyce Lyenga katika
Kijiji cha Idete.
Katika orodha hiyo pia kuna ekari 30,000 za Kampuni ya Merera Plantation Ltd katika Kijiji cha Merera.
Mashamba
mengine ni ekari 102 za Abdallah Sajiri zilizopo Kining’ina, ekari 295
za Peter Warwic zilizopo Lumemo, ekari 484.9 za Sadru Meghji zilizopo
Msolwa Ujamaa, ekari 120 za Ranifa EC &DEV. Group zilizopo Kisegese
na hekta 5,128 za Rubada zilizopo Ngalimila.
Ligazio
alitaja mashamba mengine kuwa ni ekari 2,390 za kampuni iliyokuwa ya
usafirishaji mkoani Morogoro zilizopo Mbingu, ekari 875 za Jerome
Mwakifuna zilizopo Idete, ekari 656 za Priva Mtemanyanja zilizopo
Lungongole na ekari 1,500 za Ngwasi River Valley Inv. zilizopo Mlimba.
Credit: Mwananchi
Credit: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment