Watu 4, kati yao polisi 2, wamefariki baada ya bomu kulipuka kwenye gari walilolikamata na kulipeleka kituo cha Polisi Pangani usiku wa jana
Afisa polisi akilinda mojawapo ya maeneo katika jiji la Nairobi ambalo usalama wake unatatiza. Lakini ilivyotokea inaripotiwa na gazeti la Standard, kwamba polisi hao wawili walikamata washitukiwa na na kuamua kuwapeleka kituo cha polisi wakiwa na bomu hilio.
Kabla ya kufika kituoni bomu hilo lililipuka na kuua wote, polisi pamoja na washitukiwa ambao walikuwa kwenye jaribio la kujitoa muhanga.
Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kuitambua miili ya marehemu hao, kulipatikana bomu la pili katika gari hilo baada ya mlipuko huo na wataalamu wa mabomu waliliharibu.
Usalama umeimarishwa katika eneo hilo na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi.
Thursday, April 24, 2014
BREAKING NEWS: Bomu lalipuka Kenya na kuua watu 4
Unknown
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment